
Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini mkoani Kigoma, Profesa Joyce Ndalichako
Katika Salaam hizo, Profesa Ndalichako amebainisha kuwa, Halmashauri ya mji wa Kasulu katika jimbo la uchaguzi la Kasulu Mjini inatarajia kufungua shule mpya mbili za sekondari ifikapo 2023, kufuatia serikali ya Rais Samia, kutoa fedha za kutosha kutekeleza miradi hiyo.
"Tayari tumeshaleta kiasi cha shilingi milioni 470 kwa kila kata kwa ajili ya ujenzi unaoendelea, na ninaridhishwa na hatua mbalimbali za ujenzi huu, na niwaahidi kwamba nitaendelea kutafuta fedha ili shule hizi zianze kupokea wanafunzi mwakani, milioni 130 nyingine zinatarajiwa kuwasili jimboni kwa ajili ya shule hizi, kinachotakiwa ni kuongeza kasi ya ujenzi kwa fedha zilizopo ili kuruhusu pesa nyingine kuletwa," amesema Profesa Ndalichako