Ijumaa , 1st Aug , 2014

Mwanasheria na mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu kutoka nchini Kenya Profesa PLO Lumumba, kesho ataendesha mdahalo kuhusiana na mchakato wa katiba mpya.

Mwanasheria na mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu kutoka Kenya Profesa PLO Lumumba.

Katika mdahalo huo, Profesa Lumumba atapata fursa ya kutoa nasaha zake kuhusu nini watanzania wafuate kulingana na uzoefu wa mchakato huo ulivyokuwa Kenya.

Profesa Lumumba ambaye amewahi kuongoza mchakato huo nchini Kenya, atawaeleza watanzania kuhusu namna Kenya ilivyojikuta ikiingia katika machafuko na hata kusababisha vifo kutokana na kuchezewa kwa mchakato wa katiba mpya.

Akiongea na East Africa Radio leo jijini Dar es salaamleo Mwalimu wa Sheria kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam, James Jesse ambaye ni mjumbe wa kamati ya katiba ya Chama cha Wanasheria Tanganyika TLS ambao ndio waandaaji wa mdahalo huo amesema wanalenga kuzungumzia namna ya kupata katiba Bora.