Jumapili , 10th Jul , 2016

Jeshi la polisi nchini Tanzania limevitaka vyama vya siasa nchini kuacha tabia ya kupotosha taarifa za kiusalama zinazohusu katazo la jeshi hilo la mikutano na maandamano ya vyama vya siasa visivyokuwa rasmi katazo lililotolewa na jeshi hilo Juni 7.

Jeshi la polisi nchini Tanzania limevitaka vyama vya siasa nchini kuacha tabia ya kupotosha taarifa za kiusalama zinazohusu katazo la jeshi hilo la mikutano na maandamano ya vyama vya siasa visivyokuwa rasmi katazo lililotolewa na jeshi hilo Juni 7 mwaka huu.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam makao makuu ya jeshi hilo na Kamishna wa Polisi Oparesheni na Mafunzo Nsato Marijani Missanzya wakati akiofafanua juu ya katazo la jeshi hilo na kusema kuwa sio kila mkutano wa kisiasa umekataliwa na Jeshi hilo.

Jeshi la Polisi limewataka wananchi na vyama vya vya siasa kuheshimu sheria za nchi huku likiendelea kusisitiza kuwa limepiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara mpaka pale hali ya usalama itakapotengamaa.