Ijumaa , 29th Sep , 2023

Kamishna wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP Suzan Kaganda amewataka askari kujiandaa na chaguzi zijazo kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ambapo amesema kila askari anapaswa kuzipitia sheria na miongozi ya uchaguzi na maswala mengine ili kutenda haki

Kamishna wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP Suzan Kaganda amewataka askari kujiandaa na chaguzi zijazo kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa na  uchaguzi mkuu ambapo amesema kila askari anapaswa kuzipitia sheria na miongozi ya uchaguzi na maswala mengine ili kukahakikisha wanatenda haki.

Kamishna Kaganda ameyasema hayo leo Septemba 29, 2023 wakati wa kikao na Askari Polisi wanawake  katika bwalo la maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa akiwasilisha taarifa ya Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya askari wanawake (IAWP) mwaka 2023 uliofanyika nchini New Zealand.

Katika hatua nyingine Kamishna Kaganda amesema dhamira ya amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Rais wa Jamhurui ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona idadi kubwa ya viongozi wanawake ndani ya Jeshi la Polisi.

Vilevile amewataka Askari kuendana na mabadiliko na matumizi mifumo ya TEHAMA huku akiwataka kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii ili kujiepusha kuingia katika vitendo vya utovu wa nidhamu.

Kwa upande wake Kamshna wa Msaidizi  Mwandamizi wa Polisi SACP Mwamini Rwantale amemshukuru Kamishana Kaganda kwa namna alivyo wasilisha mafunzo yaliyotolewa wakati wa Mkutano Mkuu uliofanyika nchini New Zealand ambapo amebainisha kuwa wasilisho hilo litawajengea uwezo  wa utendaji kazi kwa askari hao wanawake.