Ijumaa , 15th Apr , 2022

Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limesema kwamba kwa kushirikiana na LATRA litafanya ukaguzi wa kushitukiza hasa kwenye kipindi hiki cha sikukuu ili kuwabaini wale wanaopandisha nauli za mabasi kiholela.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoani humo Simon Maigwa, wakati wa ukaguzi wa mabasi yanayofanya safari za masafa marefu kutoka katika kituo kikuu cha mabasi cha Moshi mkoani humo.

Ambapo katika ukaguzi huo baadhi ya mabasi yamebainika kuwa na hitilafu katika mifumo ya breki na injini na kusababisha kuzuiwa kuendelea na safari hadi pale yatakapofanyiwa matengenezo na kukaguliwa upya.