Alhamisi , 3rd Nov , 2022

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, linawashikilia Askari watano wa Jeshi hilo kwa tuhuma za kujihusisha na usafirishaji wa wahamiaji haramu raia wa Ethiopia kuwapeleka nchini Malawi kupitia mpaka wa Kasumulu uliopo wilayani Kyela.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,Kamishna Msaidizi wa Polisi,  Benjamin Kuzaga,

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,Kamishna Msaidizi wa Polisi,  Benjamin Kuzaga, amethibitisha kukamatwa kwa Askari hao.

Aidha Kuzaga ametoa wito kwa Askari kuacha kujihusisha na vitendo vya usafirishaji  wa wahamiaji haramu.