
Kamanda wa polisi mkoani Tanga ACP Frasser Kashai
Jeshi la polisi mkoani Tanga limewatahadharisha viongozi na wafuasi wa vyama vya siasa mkoani humo kuwa yeyote atakayebainika kuwa na viashiria vya kufanya kampeni siku ya zoezi la kupiga kura, vitisho pamoja na kuvaa sare za chama chake kuashiria kukifanyia kampeni ya ushindi atakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Kamanda wa polisi mkoani Tanga ACP Frasser Kashai amesema wapo baadhi ya wafuasi na viongozi wa vyama vya siasa wamekuwa wakitumia baadhi ya watu kufanya kampeni ambazo ni kinyume cha sheria na taratibu za uchaguzi ambazo mara kwa mara zimekuwa zikiharibu zoezi hilo na kuleta migogoro baina ya chama kimoja
Amewataka wananchi wanapofika kituo cha uchaguzi kuhakisha kuwa wanapiga kura na kurudi majumbani kwa ajili ya kusubiri matokeo na kutahadharisha kuwa yeyote atakayebainika kufanya vurugu katika kituo cha kupiga kura wananchi wanapaswa kutoa taarifa mapema kwa askari ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.