Jumatatu , 21st Oct , 2024

Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro linawashikilia watu kadhaa kwa makosa mbalimbali ya kihalifu ikiwemo ujangili pamoja na uwindaji haramu.

Kamanda Jeshi la Polisi Mkoa Morogoro Alex Mkama amesema Jeshi la Polisi limemkamata Hassan Nalyotyo (20) mkazi wa wilaya ya kilombero akiwa na silaha aina ya Gobole na maganda saba ya risasi aina ya short gun ambavyo amekuwa akitumia katika ujangili kuwinda wanyama pori ambapo Nalyoto alikuwa na nyara za serikali ikiwemo nyama ya Kongoni, sikio, nyama ya mkia wa Tembo.

Aidha kamanda wa jeshi la polisi amesema wamewakamata watu wawili Ramadhani Pangala (38) mkazi wa Temeke, Dar es Salaam pamoja na Aloyce Mda (52) mkazi wa Manyoni Singida ambao wamekamwatwa na vipande vya meno ya tembo ambavyo walikuwa wanavisafirisha kutokea mkoani Morogoro.

 Sambamba na hilo kamanda wa jesho la polisi mkoa wa morogoro amesema jeshi la polisi limeendelea na msako wa kuwasaka madereva wanaofanya makosa hatarishi barabarani ambapo mesema katika operesheni hiyo madereva 34 wamekamatwa na leseni zao kufungiwa. Ambapo amesema baadhi ya makosa hayo ni kuendeha gari magari wakiwa wamelewa na makosa mengine kama mwendo uliopitiliza.