Ijumaa , 24th Nov , 2023

Watumishi wa Jeshi la Polisi nchini wametakiwa kutoa huduma kwa kutenda haki sambamba na kutoa huduma bora kwa wananchi wanaowahudumia ili jamii ifurahie huduma za Kipolisi hali ambayo itasaidia katika kudhibiti matukio mbalimbali ya kihalifu.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Kaspar Kaspar Mmuya

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Kaspar Kaspar Mmuya, wakati akifungua rasmi Kikao cha Kumi na sita cha baraza la wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi ambapo pia amesema kuwa, hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan ameliwezesha Jeshi la Polisi kwa kulipatia vitendea kazi ikiwemo magari kwa ajili ya kuongeza ufanisi mahala pa kazi pia amewataka watumishi hao kudumisha nidhamu na kutunza siri.

Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchin IGP Camillus Wambura, wakati akimkaribisha Katibu Mkuu kufungua Kikao hicho amesema hali ya usalama nchini ni shwari na kwamba uhalifu umeendelea kudhibitiwa na wahalifu kufikishwa mahakamani hali ambayo imechangia kuongezeka kwa idadi ya watalii nchini.