Ijumaa , 12th Aug , 2022

Pacha Rehema aliyesalia kati ya mapacha wawili waliotenganishwa Julai 01,2022, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili amefariki dunia jana Agosti 11, 2022, wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali hiyo.

Pacha Neema na Rehema

Pacha mwenzake aitwaye Neema alifariki Julai 10 mwaka huu, baada ya hali yake kubadilika ghafla akiwa ICU, na Rehema amefariki dunia siku 32 baadaye tangu kifo cha pacha wake.