Jumatano , 13th Apr , 2016

Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Mhe. Charles Mwijage, amepokea ujumbe wa wafanyabishara zaidi ya 100 kutoka nchini Oman wanaokuja kufungua fursa za kibiashara nchini katika nyanja tofauti.

Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Mhe. Charles Mwijage

Akiongea mara baada ya kumpokea Waziri wa Viwanda na Biashara wa Oman, Al Maoud Al Sunaid, amesema ujio huo ni muendelezo wa mahusiano baina ya nchi mbili ambapo kati ya sehemu watakazoangazia ni kuongeza thamani ya mazao na ukanda huru wa uwekezaji.

Mhe. Mwijage amesema falsafa ya Tanzania kwa sasa ni kutokuuza nje ya nchi mazao ghafi na badala yake serikali imejipanga kuzalisha zaidi kuchakata mazao na kuongeza thamani ili yaende moja kwa moja sokoni.

Aidha, Mhe Mwijage amesema watatumia fursa hiyo kutoka kwa wafabiashara hao ambao wanafani mbalimbali kuweza kukuza sekta ya kilimo pamoja na uwekezaji ili kufikia malengo endelevu kupitia sekta ya viwanda na biashara nchini.

Sauti ya Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Mhe. Charles Mwijage akizungumzia ujio wa wafabiashara kutoka Oman