Alhamisi , 11th Dec , 2014

Vurugu za wananchi kufunga barabara katika eneo la Dumila zimesababisha madahara baada ya nyumba Tano za kulala wageni zinazomilikiwa na wafugaji katika mji mdogo wa Dumila wilayani Kilosa mkoani Morogoro kuharibiwa.

Vurugu za wananchi kufunga barabara katika eneo la Dumila zimesababisha madahara baada ya nyumba Tano za kulala wageni zinazomilikiwa na wafugaji katika mji mdogo wa Dumila wilayani Kilosa mkoani Morogoro kuharibiwa vibaya na kuibiwa samani za ndani.

Wakizungumza kwa masikitiko wamiliki wa nyumba hizo ambapo ni wafugaji wamelalamikia kuwa hii ni mara ya pili wananchi kufunga barabara kisha kuvamia nyumba zao na kuziharibu na kusababisha hasara ambapo wameomba serikali kutenda haki kwani walihimizwa wapunguze mifugo na wawekeze katika majumba lakini kwa sasa wanachoshwa na uonevu unaoendelea na kuomba hatua zichukuliwe.

Katika hatua nyingine mji wa Dumila umeonekana shwari hakuna vurugu zozote huku wananchi wakiendelea na shughuli zao ambapo baadhi ya wafanyabiashara wakiwemo mama lishe wamelalamikia vurugu zilizotokea zimesababisha hasara na kushindwa kuuza vyakula na maduka yalilazimika kufungwa kutwa nzima.

Kamanda Polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amesema hali ni shwari katika mji wa Dumila na ulinzi umeimarishwa huku wakiendelea na uchunguzi wa waliohusika na tukio hilo na kuomba mamlaka husika kushughulikia na kumaliza mgogoro huo wa wakulima na wafugaji ili kuepusha madhara yanayotokea kwa wananchi.