Jumanne , 8th Nov , 2016

Utambulishwaji wa noti za hati fungani za nchi ya Zimbabwe umezusha hofu huku benki za nchi hiyo zikikabiliwa na wimbi kubwa la raia wa nchi hiyo wanaotoa fedha benki kwa kuhofia mfumuko mkubwa wa bei.

Noti Mpya Zimbabwe

 

Taifa hilo linalokabiliwa na ukata linatarajia kutambulisha noti zake hizo ambazo zimepingwa mno na watu, na kuibua kumbukumbu mbaya ya mwaka 2009 wakati watu waliposhindwa kuweka akiba benki kutokana na mfumuko wa bei wa asilimia milioni 231.

Maelfu ya watu nchini Zimbabwe wamekuwa wakilala nje mashine za kutolea fedha za mabenki (ATM) wakingojea kutoa fedha zao, wengi wao ikiwa ni za dola ya Marekani ambayo imekuwa ikitumika kwa sasa nchini humo.