
Mkurugenzi Mkuu na Mtendaji Mkuu wa NMB Bi. Ineke Bussemaker
Hayo yameelezwa jana na Mkurugenzi Mkuu na Mtendaji Mkuu wa NMB Bi. Ineke Bussemaker wakati akiongea na wahariri wa vyombo vya habari ambapo amesema pia mtandao wa benki hiyo nao umeongezeka na kufikia matawi 173 na kutoa huduma kwa asilimia 98 za wilaya zote nchini.
Bi. Busemaker amesema benki hiyo inasukumwa kupanua wigo wake wa kutoa huduma kutokana na kutambua umuhimu wa kuwafikishia huduma za kifedha makundi mbalimbali ya wananchi katika kuleta maendeleo.
Amesema kwa Tanzania ambayo ina watu wanaokaribia milioni 50 si rahisi kwa benki yake pekee kuwafikishia huduma za kifedha wananchi wote hivyo ni jukumu serikali pia kusaidia katika kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa na huduma za kifedha