Alhamisi , 7th Jul , 2022

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, amejiuzulu wadhifa wake hii leo na kusema anahuzunika kuacha kazi bora zaidi duniani.

Waziri Mkuu wa Uingereza aliyejiuzulu, Boris Johnson

Akizungumza wakati wa hotuba yake Boris amesema kwamba, amekubaliana na Mwenyekiti wa wabunge wa viti maalum kwamba mchakato wa kumchagua kiongozi mpya uanze na ratiba itatolewa wiki ijayo.

"Ninataka ujue jinsi ninavyohuzunishwa kuacha kazi bora zaidi duniani," amesema Boris Johnson

Aidha kabla ya kutangaza kujiuzulu, Boris leo ameteua Baraza la Mawaziri na kwamba ataendelea kuongoza hadi kiongozi mpya atakapochaguliwa.

Jaribio la kumng’oa madarakani lilianza baada ya picha na ushahidi wa mikutano na sherehe katika ofisi za serikali kubainika kufanyika wakati serikali yake mwenyewe Boris Johnson  ilikuwa imeweka sheria kali z  kuzuia mikusanyika wakati wa janga la COVID-19.