
Mbunge wa Moshi Vijijini Anthony Komu.
Akifafanua adhabu aliyopewa na chama chake kupitia maamuzi ya kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambayo imemtaka kutogombea nafasi yoyote kwenye chama hicho.
Anthony Komu amesema “Kwanza mimi ni mbunge, unavyoambiwa umepokonywa nyadhifa umenyimwa kugombea nafasi yoyote ya kichama, lakini hujanyimwa kufanya majukumu yako ya kibunge, kwa hiyo ukipewa nafasi ya kufungiwa unakuwa na wasaa mzuri wa kueneza chama chako kama mwanachama wa kawaiada”.
Ameongeza kuwa “maamuzi yalitokana na ule ujumbe unaweza kutafsiri utakavyo, na chama kimetafsiri na adhabu tumepewa kwenye uwazi (public), nafurahia maisha ya adhabu kwa sababu ni kitu nilichokikubali.”
Mapema mwezi huu Mbunge huyo akiwa na Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea waliomba msamaha pamoja na kuadhibiwa kwa kuvuliwa nyadhifa zao ndani ya CHADEMA kwa makosa mbalimbali ikiwemo kupanga njama za kumuhujumu moja ya kada wa chama hicho.