
Mbunge Viti Maalum, Agnes Marwa
Agnes amesema kampeni ya Namthamini imemgusa moja kwa moja kwa sababu fedheha za watoto wa kike wa kijijini wanazopitia anazifahamu na kuongeza kwamba yeye ni muhanga aliyewahi kupata mateso pale alipokosa taulo za kujisitiria wakati wa hedhi.
Agnes amesema wakati anaingia katika siku zake kwa mara ya kwanza hali hiyo ilimtokea akiwa shuleni, na hakuwa na vifaa vya kujisitiri kutokana na umasikini uliokuwepo nyumbani kwao.
"Baada ya kusikia kampeni hii ilinigusa sana na kunikumbusha kipindi hali hii imenikuta kwa mara ya kwanza, nilifedheheka sana kwa kuwa ilinikuta shuleni, na wakati huo hata kupata vifaa vya kujisitiria haikuwa kazi rahisi kwa kuwa umasikini ulikuwa mkubwa nyumbani, niliiba nguo ya ndani ya mama kujisitiria lakini bado haikunisaidia" Marwa.
Mbunge Agnes Marwa
Kutokana na tatizo hilo kuwa na athari kubwa kwa mabiti, mbunge huyo ameitaka jamii nzima ya watanzania kuunga mkono kampeni ya 'Nathamini' inayoendeshwa na kampuni ya East Africa Limited ikishirikiana na taasisi ya Haki za Wanawake (HAWA) iwafikie mabinti wengi zaidi nchini.
Amesema endapo kampeni hiyo itafanikiwa, itasaidia mabinti hao kukuzwa katika mazingira ya furaha watafikia malengo na hata kuwa viongozi wakubwa wa taifa.
"Siyo kwamba nina fedha nyingi sana lakini nimeona ni vyema kutoa sehemu ya mshara wangu kuelekea siku ya wanawake nimthamini mtoto wa kike hata kama nitakunywa maji na mkate sintojali" - Alisema Marwa huku akikabidhi mchango wake
Msikilize hapa alipokuwa kwenye kipindi cha Weekend Breakfast cha EA Radio