Jumanne , 9th Jun , 2015

Tume ya uchaguzi NEC yasema imebaini watu waliojiandikisha zaidi ya mara moja katika mikoa mitano ambako zoezi hilo limekamilika.

Akithibitisha taarifa hizo, mkuu wa TEHAMA kutoka Tume hiyo Dkt Sisti Cariah amesema kuwa mkoani Njombe tume hiyo imebaini majina ya watu zaidi ya 100 waliojiandikisha zaidi ya mara moja, na kwamba watu hao watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kukamatwa na kufunguliwa mashitaka.

Dkt Cariah amesema tume hiyo ina mitambo madhubuti ambayo ina uewezo wa kutambua aina yoyote ya udanganyifu na kuwataka wananchi wasithubutu kufanya vitendo vya udanganyifu kwa kuwa ni kinyume cha sheria na adhabu yake ni kifungo au faini au vyote kwa pamoja.

Mikoa ambayo tayari zoezi hilo limekamilika ni Njombe, Mtwara, Ruvuma, Lindi na Iringa ambako takriban watu 2,984,000 wameandikishwa.

Msikilize hapa Dkt Cariah akielezea kwa kina kuhusu taarifa hizo