Jumatano , 5th Jan , 2022

Mchambuzi wa siasa nchini Goodluck Ng'ingo, amesema iwapo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, hatobadilika na kuendelea na utaratibu wake wa kukosoa hadharani nje ya kufuata utaratibu jambo ambalo litakuwa na manufaa kwa pande zote mbili ni yeye kuachia ngazi.

Mchambuzi wa siasa nchini Goodluck Ng'ingo, na kulia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 5, 2022, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio, kufuatia Rais Samia kuonesha kukerwa jana kutokana na Spika Ndugai kukosoa hadharani kuhusu mkopo wa trilioni 1.3 uliotolewa na IMF.

"Kama Spika ataendelea na utaratibu wake wa kukosoa hadharani bila kufuata utaratibu, jambo ambalo litakuwa na manufaa kwa pande zote mbili ni yeye kuachia ngazi, yeye kwa nafasi yake maoni anayotoa yanachukuliwa kwa uzito na hasa kwa sababu wengi wanaamini yeye anaweza kuwa na taarifa zote muhimu," amesema Ng'ingo.