Jumamosi , 2nd Jan , 2016

Waziri wa Kilimo, mifugo na Uvivu, Mhe. Mwigulu Nchemba amewafukuza kazi Mkuu wa mnada wa Pugu na watumishi waliokuwa zamu kuanzia tare 24 mwezi 12 mwaka jana hadi tarehe 1 mwaka huu kutokana na kuwepo kwa ubadhirifu wa ukwepaji kodi.

Waziri wa Kilimo, mifugo na Uvivu, Mhe. Mwigulu Nchemba, Waziri wa TAMISEMI Mhe. George Simbachawene, na Naibu waziri wa afya jinsia , watoto na wazee Dkt. Hamis Kigwangala wakiteta jambo baada ya kutembelea mnada wa Pugu na machinjio ya vingunguti

Akiongea leo Jijini Dar es Salaam baada ya kufanya ziara na Mawaziri wengine wawili Akiwemo wa TAMISEMI,Mhe. Nchemba amesema kuanzia sasa watafute kazi nyigine,na wahakikishe wanafika ofisi ya Katibu mkuu wizara ya mfiguo mapema Jumatatu tar.04/01/2016.

Aidha Waziri huyo amesema kuanzia sasa serikali imesitisha uchukuaji wa Ushuru eneo la mnada wa pugu,badala yake makusanyo yote ya fedha za serikali hizo yatafanyika Machinjio ya Vingunguti kwa kutumia mashine za Elektroniki za EFD,na mnada wa pugu utakuwa unatumika kutoa vibali tu vya mifugo ilikudhibiti ubora wa mifugo inayopaswa kuchinjwa.

Katika hatua nyingine amesema kuwa eneo la kuhifadhia nyama lililokuwa limejengwa kwa fedha za Wananchi kushirikiana na serikali lifunguliwe kwaajili ya Wananchi kulitumia kuhifadhia nyama hiyo,Awali eneo hilo lilifungwa bila sababu za msingi.

Aidha Mh. Mwigulu amesema kuwa umeme uliokuwa umekatwa eneo hilo urudishwe hii leo kwa ajili ya kuwarahisishia wananchi shughuli zao huku akiita Halmashauri ya ilala kuboresha miundombinu ya Machinjio hayo.

Kwa upande wake Naibu waziri wa afya jinsia , watoto na wazee Dkt. Hamis Kigwangala amewataka Madaktari waliokuwa na jukumu la kuthibitisha mifugo hiyo kama inafaa kwa matumizi ya binaadamu kupisha uchunguzi kwani kumeonekana kuwepo na wanyama wasiofaa kuliwa na binaadamu machinjioni hapo