Jumapili , 21st Jul , 2024

Mbunge wa kuteuliwa na Rais na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk hii leo Julai 21, 2024, ameandikia barua ya kujiuzulu nafasi yake ya ubunge kwenda kwa Spika wa Bunge la  Tanzania, Dkt. Tulia Ackson.

Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk,

Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya Bunge iliyotolewa hii leo imeeleza kuwa, mbunge huyo wa kuteuliwa amefikia uamuzi huo kufuatia changamoto za kijamii zinazomkabili kwa sasa.

"Ninalazimika kuchukua uamuzi wa kujiuzulu ili nipate nafasi ya kushughulikia changamoto hizo," imeeleza barua Mhe. Mbarouk katika barua yake ya kujiuzulu Ubunge.