
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (CDF), Jenerali Venance Mabeyo (Kushoto), Kulia ni wanajeshi wakiwa wamebeba mwili wa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Marehemu Elias John Kwandikwa.
Akizungumza katika zoezi la kuaga mwili wa Marehemu Kwandika, Jenerali Mabeyo ameshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyoguswa na msiba huo mzito huku akiweka wazi kuwa ni nadra sana kuwapata binadamu wenye sifa adimu kama alivyokuwa nazo marehemu Kwandika.
“Marehemu Elias Kwandikwa alikuwa ni mtu wa kipekee, upekee wa kwanza ni upole wake, usikivu na unyenyekevu wake, upole wake huu uliwahi pia kuelezwa na Hayati Dkt. John Magufuli mara baada ya kumuapisha kuwa Waziri wa Ulinzi, na sisi tuliobahatika kufanya kazi chini yake ni mashahidi wa hilo,” ameswema CDF Mabeyo.
Akielezea ufanisi wa marehemu katika kufanya kazi Jenerali Mabeyo amesema watamkumbuka kwa ufanisi na jitihada zake katika kulisimamia na kutatua changamoto za jeshi hususan katika huduma ya afya jeshini pamoja na faraja zake kwa wasataafu.
“Marehemu Kwandikwa ni aina ya kiongozi asiyependa kutumia muda mwingi ofisini alipenda kuwatembelea maafisa ili aweze kujionea mazingira halisi ya ufanyaji kazi, aliweza kuwatembelea hata waastafu wetu nia kubwa nikufahamu maisha yao baada ya kustaafu kweli alitutia faraja kubwa hata sisi tuliokuwa kazini,” amesemsa Jenerali Mabeyo.
Naye Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu amemuelezea marehemu Kwandikwa kuwa miongoni mwa watu waliotakiwa kupata sifa za uadilifu si tu kwa uongozi wake bali ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Marehemu Elias John Kwandikwa alizaliwa mnamo tarehe 1/07/1966 katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga na kufariki dunia tarehe 2/08/2021 katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu, na ameacha mke, watoto pamoja na wajukuu.