Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu
Katika uzinduzi huo Rais Samia amesema ujenzi wa barabara hiyo, ulianza chini ya Rais wa Awamu ya Tano Hayati John Magufuli na angetamani leo aone matunda ya jitihada zake lakini hayupo hivyo watanzania wamuombee pumziko la amani.
Aidha mapema kabla ya Rais Samia kuzungumza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame M. Mbarawa alieleza kuwa upanuzi wa barabara hiyo ya Morroco - Mwenge yenye urefu wa Kilometa 4.3 umefanywa kwa fedha za msaada kutoka Japan jumla ya shilingi bilioni 71.85 za kitanzania.
Zaidi tazama Video hapo chini