Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara nchini, Johnson Minja.
Kesi hiyo ambayo inasikilizwa katika mahakama ya Wilaya ya Dodoma inategemewa kukusanya watu wengi hasa wafanyabiashara nchini ambao tangu mwenyekiti huyo alipopandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Januari 28 mwaka huu, wamekuwa wakifunga maduka yao kwa ajili ya kuja Dodoma kusikiliza kesi ya mwenyekiti wao.
Aidha kesi hiyo imevuta usikivu wa watu wengi pale mahakama ya Wilaya ya Dodoma ilipofutia dhamana yake Machi 26 kwa kile kilichodaiwa mahakamani hapo kuwa Mwenyekiti huyo amekuwa akiendelesha mikutano ya kuwazuiaya wafanya biashara nchini kugomea matumizi ya mashine za kukusanyia kodi za Efds.
Hata hivyo baada ya kukaa rumande kwa siku sita baada ya kufutiwa dhamana, April mosi mwaka huu mwanasheria wake, Godfrey Wasonga aliiambia mahakama kuwa hoja hiyo haina mashiko kwani sheria inasema kama alifanya kosa hilo angekamatwa muda huohuo na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria jambo ambalo halikufanyika.
Ambapo hakimu mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Dodoma, Rhoda Ngimilanga alimwachia mshtakiwa huyo ili aendelee kuwa nje kwa dhamana baada ya kujiridhisha kuwa mtuhumiwa huyo hakuvunja masharti ya dhamana yake tangu alipoachiwa kwa dhamana Januari 28 mwaka huu.