Jumatano , 10th Aug , 2022

Elizabeth Cheleo mwenye umri wa miaka 37 mkazi wa mtaa wa Nsemulwa, Kata ya Nsemulwa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, amepoteza maisha kwa kujinyonga chumbani kwake  kwa kutumia kipande cha kitenge alichokining'iniza juu ya kenchi.

Kitenge

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi Ali Makame Hamad, na kusema kwamba baada ya uchunguzi jeshi hilo lilibaini kwamba marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa akili.