Jumapili , 13th Jul , 2014

Mkuu wa Majeshi nchini Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange amewataka wananchi waishio pembezoni mwa Ziwa Nyasa kuondoa wasiwasi kutokana na mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi.

Mkuu wa Majeshi nchini Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange.

Mwamunyange ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Liuli wilayani Nyasa wakati wa ziara ya kutembelea vikosi na viteule vya jeshi mkoani Ruvuma.

Mkuu wa Majeshi Mwamunyange amewataka wakazi wa maeneo hayo kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa taifa bila kuwa na hofu kwamba machafuko yoyote yanaweza kutokea.

Jenerali Mwamunyange amesema mgogoro wa mpaka ni changamoto ya muda mrefu inayoshughulikiwa na serikali za nchi zote zilizo kwenye mgogoro huo ambapo amewataka askari wanaounda vikosi hivyo kuishi vizuri na wakazi wa wilaya ya Nyasa ili uwepo wao usitafsiriwe kuwa ni ugomvi bali ni sehemu ya jeshi kulinda nchi na mipaka yake.