Alhamisi , 23rd Jun , 2022

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar Salum Mwalimu, amesema kwamba kulingana na hali ya maisha kuwa juu kwa miaka miwili sasa imepelekea watoto wa Kizanzibar kuvaa nguo za mitumba nyakati za sikukuu, utaratibu ambao hapo mwanzo haukuwepo.

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar Salum Mwalimu

Kauli hiyo ameitoa hii leo Juni 23, 2022, jijini Dar es Salaam, wakati akiichambua bajeti ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

"Maisha yetu Wazanzibar ni Eid, ni moja kati ya matukio makubwa sana na tumezoea kununuliana nguo wakati wa sikukuu ya Eid, Wazanzibar tulikuwa hatuijui mitumba, mitumba labda tukija huku tukiiona ndiyo tunanunua, miaka hii miwili watoto wa Kizanzibar sikukuu ya Eid wanavaa mitumba, nguo hazishikiki,"amesema Mwalimu