Alhamisi , 16th Mar , 2023

Mtoto wa kiume wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Jeneral Muhoozi Kainerugaba, ameweka wazi nia yake ya kugombea urais wa Taifa hilo katika uchaguzi mkuu wa Taifa hilo mwaka 2026.

Jeneral Muhoozi Kainerugaba

Jenerali Muhoozi, kupitia ukurasa wa  mtandao wa twitter ameweka ujumbe huo huku akidhihirisha kwamba ni majibu kwa wale waliokuwwa wakihoji swala la yeye kugombea urais.

“Mmenitaka mimi kulisema daima! Sawa, kwa jina la Yesu Mungu wangu, kwa jina la vijana wote wa Uganda na dunia na kwa jina la mageuzi bora, nitagombea Urais katika mwaka 2026!” Ulisomeka  ujumbe huop katiaka ukurasa wake wa Twitter.

Tetesi za Jenerali Muhoozi kuandaliwa kumrithi baba ya Yoweri  Museven zilianza miaka 10 iliyopita huku yeye Jenerali akikanusha kwa kudai Uganda sio nchi ya Kifalme

Mwezi Juni 2013 Jenerali Muhoozi alijitokeza na kupinga tetesi hizo na kusema: "Uganda sio nchi ya kifalme ambao uongozi unarithishwa kutoka kwa baba kwenda kwa mtoto. Hili linalosemwa ni Muhoozi ni ‘mradi’ ni maneno tu yakutungwa na watu."