
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoani Mbeya ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama Juma Homera amesema watuhumiwa hao (Majina yana hifadhiwa) walikamatwa Novemba 11, 2023 majira ya saa 6:00 usiku na kikosi kazi cha madini.
Homera amesema vipande hivyo vya dhahabu 28 vina uzito wa kilogramu 1.08373 dhamani yake ni shilingi mil.142.229 za kitanzania mrabaa ukiwa ni shilingi milioni nane, ada ya ukaguzi, milioni 2,844,5866.36 kodi ya huduma shilingi 426,687.96 na kodi ya zuio shilingi milioni 13.231.
Homera amesema kuwa wizi huo unasababisha upotevu wa takwimu halisi za uzalishaji wa madini ya dhahabu na hatimaye kupunguza mchango wa sekta hiyo kwenye pato la Taifa na kwamba wahutumiwa wote wawili wanashilikiwa kituo cha Polisi Mbeya na wamefunguliwa jadala MBE/IR/5162/2023 kwa ajili ya mahojiano zaidi.