Jumanne , 3rd Mei , 2016

Mtoto wakike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu ameokolewa akiwa hai jana kutoka kwenye kifusi cha jengo la ghorofa lililoanguka Jijini Nairobi baada ya siku nne kupita.

Mwanajeshi akisaidia na mbwa kutafuta watu waliofukiwa na kifusi cha jengo Jijini Nairobi

Mtoto huyo aliokolewa jana majira ya saa kumi alfajiri, na kukimbizwa katika hospitali ya taifa ya Kenyatta.

Kamanda wa Kitengo cha Kukabiliana na Majanga, Pius Maasai, ameviambia vyombo vya habari nchini humo kuwa mtoto huyo yupo kwenye hali nzuri.

Kamanda wa Kaunti ya Nairobi, Japheth Koome, amesema kitendo cha kumuokoa mtoto huyo akiwa hai kimewapa matumaini waokoaji kupata watu wengine zaidi waliohai.