Nyumba ikiwa imezungukwa na maji yaliyotokana na mvua kunyesha
Akizungumza na EATV Kamanda wa kikosi cha zimamoto na uokoaji Mkoa wa Kagera, Hamis Dawa amesema , walipata taarifa jana saa moja usiku kutoka kwa Askari wa Zimamoto waliokuwa doria.
Askari hao walidai kuwa wameuona mwili wa mtoto katika dimbwi la maji eneo la Nyamkazi katika Manispaa ya Bukoba, na kulazimika kwenda kuuopoa.
Dawa amesema mazingira yanaonesha mtoto huyo alitumbukia katika dimbwi wakati akicheza, na kuwa Mama mzazi wa mtoto huyo Gisela Mwombeki akiwa hafahamu mahali alipoenda mtoto wake.
Tazama zaidi