Jumatano , 21st Sep , 2022

Mtoto aliyetambuliwa kwa jina la Enock Melita (4) mkazi wa kijiji cha Kiru Six kitongoji cha Ndoroboni wilayani Babati mkoa wa Manyara ameuwawa  kikatili  na  shangazi yake anayejulikana kwa jina la Nembris Melita na kisha kumbeba na beseni la kufulia nguo na kumtupa pembezoni mwa mto

 

Mama mzazi wa mtoto huyo Upendo Lendoya amesema mtoto wake ameuawa na wifi yake na hana la kufanya anatafakari kilichotokea.

Wakazi wa kijiji hicho wamegoma  chakula kupikwa kwenye msiba huo kutokana na mauwaji ya kikatili yaliyofanyika kwa mototo huyo na kutokuwa na ushirikiano wa ndugu wa marehemu 

Naye Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara George Katabazi amesema uchunguzi bado unaendelea na pindi utakapo kamilika mtuhumiwa atapewa haki yake huku mwakilishi wa dawati la jinsia akihamasisha Amani itawale kwenye kijiji hicho hadi upelelezi ukamilike