Jumanne , 21st Jul , 2020

Wakazi wa kituo kipya Gongolamboto wameiomba Serikali kukamilisha ujenzi wa Mtaro wa kupitisha maji taka ambao awali ulichimbwa na kuachwa bila kukamilishwa kwa ujenzi wake licha ya kujengwa kwa baadhi ya vivuko.

Pichani Hali ilivyo katika kituo kipya Gongolamboto baada ya kukosekana mtaro wa majitaka

Wakazi wa kituo kipya Gongolamboto wameiomba Serikali kukamilisha ujenzi wa Mtaro wa kupitisha maji taka ambao awali ulichimbwa na kuachwa bila kukamilishwa kwa ujenzi wake licha ya kujengwa kwa baadhi ya vivuko.

Mara baada ya Eatv kutembelea katika eneo Hilo limeshuhudia na kuzungumza na Wakazi hao ambao wameelezea jinsi wafanyabiashara wadogo wanavyotupa taka na kusukumia mtaroni humo taka hizo ambazo zote husombwa na maji kuletwa kwao hasa katika kipindi Cha mvua.

Wamesema Mtaa huo kwa Sasa Hali ya kiafya ni Tete kutokana na maji machafu yasiyoisha Ambapo zaidi ya nyumba 150 zimeathirika.

"Ukweli tumepeleka malalamiko yetu katika uongozi kwa kipindi kirefu lakini mpaka sasa hakuna utatuzi,heri mmefika walau linaweza kutatuliwa" ameeleza Sophia Ramadhani mkazi wa Gongolamboto.