Alhamisi , 24th Nov , 2022

Mtanzania na Mhandisi wa masuala ya umeme aliyegundua WAGA Power Pack Gibson Kawago, amechaguliwa na Chuo cha Uhandisi cha Uingereza kushiriki katika tuzo za Afrika 2023 za ubunifu wa uhandisi (APEI).

Gibson Kawago

Kupitia taarifa ya chuo hicho imesema  kuwa Gibson Kawago kutoka Tanzania ni miongoni mwa washiriki waliochaguliwa ambapo mwaka huu nchi kumi zinashiriki kutoka Afrika ikiwemo Tanzania,  Angola,Cameroon,Ethiopia,Ghana Nigeria, Sierra Leon,Afrika Kusini, Uganda na Zimbabwe.

Aidha lengo la Tuzo hizo ni kuendeleza wabunifu wa Kiafrika na kuendeleza bunifu zao ambapo mshindi wa kwanza atajishindia zaidi ya milioni 60 huku lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto katika maendeleo endelevu ikiwemo elimu bora, afya bora na ustawi na nishati safi.

Mtanzania Gibson kawago ni mvumbuzi wa WAGA Power Pack ambapo anakusanya betri za laptop kisha anazichaji na kutengeneza umeme wa jua,umeme wa baiskeli, umeme wa biashara na majumbani.