Jumatatu , 29th Oct , 2018

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassani amewataka watanzania kujenga utaratibu wa kupenda bidhaa zinazozalishwa nchini lengo likiwa ni kuwatia moyo wazalishaji wa ndani kwa nia ya kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan

Samia Suluhu amezungumza hayo wakati akifungua wiki ya maonesho ya viwanda Mkoani Pwani ambayo yaliyoandaliwa na mkuu wa mkoa, Injinia Evarist Ndikilo akishirikiana na taasisi nyingine za umma na binafsi.

Ninawahasa watanzania tupende vya kwetu kwa kujenga utamaduni wa kutumia bidhaa zinazozalishwa na wawekezaji wa ndani, niwaombe pia wazalishaji kutumia utaratibu wa serikali kuuza bidhaa ambazo kwa ndani mnatakiwa kuuza bidhaa asilimia 20 na nje asilimia 80.” Amesema Makamu wa Rais

Aidha Makamu wa Rais, Samia ameongeza “kingine niwaombe wawekezaji msipigane vita wenyewe kwa wenyewe kila mtu yuko nchini kisheria, kila mmoja amekaa kwa nafasi yake soko litachagua nani ataenda huku mkuu wa mkoa nakuachia lishughulikie”.

Aidha Samia amewataka wamiliki wa viwanda kutumia malighafi ambazo zinazalishwa nchini ili kuleta ajira kwa wazawa.