
Katika taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Tanzania imeeleza mambo hayo kama ifuatavyo
Kwanza Tanzania inaunga mkono hoja ya kuongeza fedha za ufadhili kwa kuzingatia athari zinazozidi kuongezeka kwa sasa na kuhakikisha ahadi ya nchizilizoendelea kutoa dola bilioni mia moja kila mwaka kwa nchi zinazoendelea kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi zinatimizwa.
Pili ni kuhakikisha mkutano unaridhia uanzishwaji wa mfuko wa kupambana na majanga na maafa yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi
Suala la tatu ni kuhakikisha juhudi za kuelekea matumizi ya nishati safi zinakuwa jumuishi njia ya kuhimiza nishati za mpito zinazozingatia usawa wa kijinsia
Na siala la nne ni kuhakikisha mjadala wa masuala ya jinsia unazingatia maadili ya kitaifa na kijamii na wanawake wanapewa kipaumbele katika hatua za kushughulikia mabadiliko ya tabianchi