Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa
Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 14, 2022, mkoani Tabora wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya serikali na shighuli zingine zenye kuliletea tija Taifa.
"Achaneni na maneno ya watu wanaochochea hivi na hivi Mh. Rais Samia halali, sisi ambao tunaomsaidia tunaona jinsi ambavyo halali akihangaika kwa ajili ya shida za Watanzania, sisi tutakuwa watu wa ajabu sana Mh. Rais halali anahangaika na sisi halafu kunaa mtu mmoja anakuja anasema vitu vya ajabu ajabu tumuunge mkono, tuwakatae watu wa namna hiyo, tumtie moyo Mama aendelee kupiga kazi atutafutie mambo mazuri," amesema Msigwa