Jumatano , 23rd Jul , 2014

Msichana anayefanya kazi za ndani aliyejulikana kwa jina la Safela Andrew mkazi wa Area C katika Manispaa ya Dodoma, amekutwa amekufa na mwili wake kukutwa kwenye nyumba ambayo haijakamilika huku ukiwa umeharibika vibaya.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma David Misime.

Maiti ya binti huyo imekutwa katika nyumba hiyo jana asubuhi huku nguo zake za ndani zikiwa kando ya maiti hiyo na hivyo kutilia shaka kuwa huenda binti huyo alibakwa kabla ya kuuawa.

Naye mwajiri wa binti huyo Jackson Coy, amesema binti huyo alipotea tangu usiku wa Julai 19 mwaka huu katika mazingira ya kutatanisha ambapo walipoona haonekani walitoa taarifa polisi.

Kwa upande wake Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limesema kuwa linafanya uchunguzi kuhusiana na kifo hicho huku ikisubiri uchunguzi wa madaktari kubaini chanzo cha kifo chake.