![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2024/04/09/Untitled-2.jpg?itok=AaEqs0Zq×tamp=1712647667)
Bidhaa hizo zimekabidhiwa kituo cha Afya Mohoro kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji ambazo ni pamoja na Dawa, za kuzuia na kutibu malaria, kuhara na yale ya mlipuko kama vile kipindupindu.
Kwa upande wa vifaa tiba ni pamoja na magodoro, mashuka na vyandarua, milingoti ya kutundikia maji tiba ( Drip Stand), Binliners na vifaa vingine vitakavyosaidia katika zoezi hili.
Akizungumza wakati wa kukabidhiwa bidhaa hizo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Dr. Hamis Abdallah.
ameishukuru MSD kwa juhudi za haraka zilizofanyika kuweza kuwafikia wahanga wa mafuriko. Ameongeza kuwa bidhaa hizo zitasaidia katika utoaji wa huduma kwa waathirika wa mafuriko. #EastAfricaTV