Jumatano , 28th Sep , 2016

Kaunti ya Mombasa inaendelea kushinikiza pendekezo lake la kutoza ushuru kwa makontena yanayosafirishwa kutoka bandarini licha ya kuwepo na upinzani kutoka kwa wasafirishaji pamoja na serikali ya Kenya.

Kati ya eneo la bandari ya Mobasa.

Kwa mujibu wa Muswada wa Fedha wa mwaka 2016/2017 kaunti hiyo ilipendekeza ushuru wa shilingi 5,000 za Kenya kwa kontena moja la futi 20, na shilingi 9,000 kwa kontena moja la futi 40.

Mtendaji Mkuu wa Baraza la Wasafirishaji Afrika Mashariki (SCEA) Gilbert Langat amepinga ushuru huo wa maendeleo ya miundombinu na kusema wakala wa usafirishaji kontena tayari wanailipa serikali kuu.