Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, wakati wa mahafali ya kuhitimu kwa vijana 500 wa mafunzo ya uwezeshaji vijana kiuchumi yaliyotolewa na VETA kwa kushirikiana na shirika la Plan International yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mhe. Mavunde amesema kuwa vijana hao wakitumia mafunzo hayo kama inavyotakiwa yana uwezo wa kubadilisha maisha yao kiuchumi pamoja na kwenda kuwasaidia vijana waliokuwa mtaani waweze kupata elimu hiyo ya biashara.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo hayo kutoka Chuo cha Ufundi (VETA), Lukindo amesema pamoja na kufanikisha mafunzo hayo bado kuna changamoto mbalimbali ambazo wanakutana nazo wakati wa mafunzo hayo.