Jumatatu , 29th Oct , 2018

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Injinia Evarist Ndikilo amesema kuwa kukosekana kwa nishati ya umeme ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili wawekezaji wa viwanda mkoani humo kwa kukwamisha uzalishaji wa viwanda.

Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wiki ya viwanda mkoani Pwani mbele ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu, mkuu huyo wa mkoa amesema licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali bado kuna changamoto ya nishati ya umeme.

Changamoto ya kwanza ni nishati ya umeme, sasa hivi mahitaji ya umeme kwenye mkoa wetu, megawats 79 zinazopatikana 62  tuna pengo la megawats 17, tunachangamoto ya nishati ya gesi, na changamoto hizi zinapelekea kukatisha tamaa juhudi za viwanda, kwenye mkoa wetu”, amesema Ndikilo.

Aidha Mkuu huyo wa mkoa amezitaja changamoto nyingine ni ubovu wa barabara, kwenye baadhi ya viwanda, changamoto ya maji, na upatikanaji wa masoko ya bidhaa zinazozalishwa.

Kuna changamoto ya barabara, lakini pia changamoto ya masoko kwa sababu baadhi ya watumiaji kutothamini bidhaa za ndani, tunahamasisha serikali kuongeza msukumo wa kumaliza changamoto ili kuhamasisha uwekezaji nchini.” Ameongeza Ndikilo