Jumatano , 9th Dec , 2015

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadick amesema wanaandaa utaratibu na wadau husika wa usafiri wa Daladala jijini Dar es Salaam, kupulizia dawa za kuuwa wadudu kwenye daladala pamoja na kuhakikisha kila daladala inakuwa na kitunzia uchafu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadiki (kuia) akifanya usafi wa jiji katika Barabara ya Kawe kwenye viwanja vya Tanganyika Packers

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam katika kituo cha mabasi yaendayo mikoni cha Ubungo ambapo ndipo alipokwenda kushiriki zoezi la usafi amesema kesho watakaa na wadau wa usafiri wakiwemo Sumatra ili kuona ni jinsi gani agizo hilo linatekelezeka.

Mh. Sadick amesema kuwa kumekua na tabia ya abiria ambao wakishamaliza kula au kwenye kwenye daladala wanatupa uchafu kiholela bila kuzingatia sheria za utunzaji mazingira, hivyo daladala zote zikiwa na vitunzia taka itasaidia katika utunzanzaji wa mazingira na kuliweka jiji Safi.

Aidha Mh. Sadick ameongeza kuwa kwa wasafirishaji wa mabasi yaendayo mikoani nao wazingatie katika kupulizia dawa magari yao, ili kuepusha kusambaza ugonjwa unaoambukizwa na bakteria wa uchafu kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

Pia amesema kuwa serikali ya mkoa wake inaanda utaratibu wa kuwaondoa watu wote wanaoshinda katika kituo hicho bila shughuli maalumu, huku akisema wengi ndio wanaongoza kwa uchafuzi katika kituo hicho