Jumatano , 4th Jun , 2014

Bunge la Afrika Mashariki linalokutana jijini Arusha nchini Tanzania jana limeshindwa kujadili na kupitisha makadirio na matumizi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kufuatia wabunge watatu kujitoa katika kikao hicho.

Mwakilishi wa Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki, Bi. Shyrose Bhanji.

Akizungumzia kujitoa kwake mmoja wa wabunge hao Shyrose Bhanji wa Tanzania amesema wamechukua uamuzi huo kwa sababu ya kutokuwepo kwa vipengele kadhaa ikiwemo kile cha kujadili uhalali wa spika wa bunge hilo Mh. Margareth Ziwa kutoka nchini Uganda kuendelea kushika wadhifa huo.

Kwa upande wake mwanasheria wa bunge hilo Wilbert Kaahwa amesema uamuzi wa kujitoa kwa wabunge hao sio halali kwa kuwa wamechelewa kusaini muswada wa kutokuwepo bungeni.