Jumatatu , 19th Mei , 2014

Fedha zinazopotea kutokana na misamaha ya kodi mbalimbali nchini Tanzania zimekuwa zikichangia kutofanikiwa kwa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba za walimu na madarasa ya shule za msingi na sekondari nchini.

Msemaji wa kambi ya upinzani kuhusu elimu, Bi. Suzan Lyimo.

Hayo yameelezwa na Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Suzan Lyimo wakati akitoa hatuba ya Makadirio ya Bajeti Kivuli ya wizara hiyo katika mwaka wa fedha 2014/2015.

Nao wabunge James Mbatia na Peter Serukamba wakichangia makadirio ya bajeti ya wizara hiyo wamesema ufaulu wa wanafunzi katika shule nchini umekuwa ukizorota kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutokuwepo kwa chombo maalum cha kusimamia elimu nchini.