Jumanne , 28th Jun , 2016

Mbunge wa jimbo la Mwibara Kangi Lugola ameiambia serikali Mjini Dodoma kwamba miradi ya maji katika jimbo lake imeshindwa kukamilika kwa muda wa miaka 7 mfulilizo huku vigezo vyote vinavyotakiwa vikiwa vimekamilishwa na Halmashauri ya Bunda.

Baada ya kutoa kero hiyo ambayo ameitoa wakati akiuliza swali la nyongeza ambapo Naibu Waziri wa maji Mhandisi Isack Kamwele amesema kinachotakiwa kwenye miradi ni 'vielelezo vinavyotakiwa vikishawasilishwa wizarani na kama mradi ulikuwa kwenye bajeti mradi huo hutekelezwa .

Hivyo kufuatia Mbunge Lugola kusema kwamba vielelezo vyote tayari Halmashauri ya Wilaya ya Bunda imekwisha wasilisha vielelezo hivyo na miradi imekwama serikali imeahidi kushughulikia jambo hilo kwa wakati.

Aidha Naibu Waziri amesema kwamba fedha kwenye miradi ya maendeleo hupelekwa kulingana na tathmini na kiwango cha uzalishaji cha miradi wenyewe.