Jumanne , 17th Jun , 2014

Kiwango cha elimu nchini Tanzania kimeonekana kushuka kutokana na serikali kuanzisha mifumo mingi ya kukuza elimu bila kuifanyia utafiti na kujipanga katika kukabiliano nayo.

Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dkt Shukuru Kawambwa.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar-es-Salaam na Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, shule kuu ya elimu Dkt. Eugenia Kafanabo na kusema kuwa serikali imekua ikianzisha mifumo mingi lakini imeshindwa kutatua tatizo la elimu.

Dkt. Kafanabo ameongeza kuwa bajeti ndogo katika sekta ya elimu ni sababu nyingine ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kushusha kiwango cha elimu nchini.