Mikoa yenye wagonjwa wa Corona yatajwa

Jumatano , 7th Jul , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona kwani mpaka sasa waathirika wa ugonjwa huo wapo maeneo mbalimbali nchini ikiwemo mikoa ya Arusha, Mwanza, Dodoma na Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameitoa hii leo Julai 7, 2021, jijini Dodoma, katika eneo la Kibaigwa akiwa njiani kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya ziara yake ya siku mbili.

"Ninaowaona wameziba midomo na pua hapa ni kidogo, nataka niwaambie tuchukue tahadhari zote dhidi ya maradhi ya Corona, wimbi la tatu lipo kwenye nchi na hakuna kuficha, tuna wagonjwa mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na mingine hata Dodoma," amesema Rais Samia.