Alhamisi , 20th Jan , 2022

Gema Haule aliyekuwa mhudumu wa nyumba ya kulala wageni iitwayo Peace lodge, iliyopo Kata ya Matarawe Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, amekutwa ameuawa kwa kukabwa shingoni na kamba ya kiatu na mtu asiyefahamika jina, ambaye alikuwa mteja katika chumba ambacho alipanga kwa siku tano.

Gema Haule, aliyeuawa

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Pili Mande, amesema kuwa tukio hilo limetokea Januari 18, 2022, majira ya saa 10:00 jioni ambapo mtuhumiwa huyo baada ya kushindwa kulipa deni la 50,000 alilokuwa akidaiwa vitu vyake vilizuiliwa na mmiliki wa nyumba hiyo na alikuwa akirudi mara kwa mara kuviulizia na ndipo alipochukua maamuzi hayo ya kikatili.

Kamanda Mande amesema, mara baada ya kutekeleza unyama huo mtuhumiwa alifanikiwa kuchukua baadhi ya vitu vyake na kutokomea, na jeshi la polisi linaendelea kumtafuta.