Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo amesema kuwa kuingia kwa megawati 235 kunafanya mgao wa umeme kupungua kwa asilimia 85 nchini.
"Ninafurahi kusema kile ambacho tuliahidi kufikia tarehe 25 Februari tutakuwa tumeingiza umeme wa mtambo namba 9 kimekamilika," amesema Dkt. Biteko.
Amesema kuwa mtambo namba 8 unatarajiwa kukamilika mwezi Machi na kufanya jumla Megawati 470 kuingia kwenye Gridi ya Taifa.
Ameongeza kuwa kazi ilipaswa kukamilika mwezi wa sita lakini kutokana na msukumo uliowekwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umefanya kazi kukamilika kabla ya wakati.